Staa mrembo kutoka Bongo Movies, amewaasa wanawake kuacha kutoa mimba hata kama watakumbana na mtatizo,kwani mtoto ndio kila kitu katika maisha.
Msanii huyu alitoa wito huo hivi juzi kati akiwataka wajawazito wote waliokataliwa na wapenzi wao kuonyesha kuwa wao ni wanawake majasiri kwa kutothubutu kutoa mimba hizo.
"Mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, siku ya leo nawashauri wanawake wanaokataliwa mimba na wapenzi wao wasitoe wala kufanya chochote muonyeshe kama wewe ni mwanamke jasiri na unaweza, mtoto ndio kila kitu, please.... usitoe mimbaaa". Alisema.
Kufuatia ujumbe huo baadhi ya mashabiki wake walionekana kumuunga mkono mrembo huyu ambae ni mama wa mtoto mmoja.
No comments:
Post a Comment