Baada ya uvumi kusambaa kuwa mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi Vengu amefariki na baadae kaka yake alikanusha uvumi huo, kiongozi wa kundi hilo Sekioni David amesema wamepata usumbufu mkubwa juu ya uvumi huo na wao kama kundi wameamua kuchukua hatua zaidi ili kukomesha tabia hiyo kwa kuwa sio mara ya kwanza, wamepata ushauri kutoka TCRA ambao wamewashauri kuchukua hatua ili kuweza kujua chanzo cha uvumi huo na kuchukua hatua zaidi kwa wahusika na muda sio mrefu mhusika atajulikana
Ni muda mrefu msanii huyo hajaonekana akiigiza pamoja na kundi lake la Orijino Komedi; “Vengu ameanza kuumwa 2011 mwezi wa tisa“
Andrew Shamba ambaye ni kaka wa Joseph Shamba a.k.a Vengu, hapa akaanza kuzungumzia jinsi tetesi hizo walivyozipokea; “Familia inatusikitsha kwa maana kwamba haina ukweli wowote hii ishu ni zaidi ya mara tano wanazungumza hao watu.. na hao watu hawazungumzi kwa mapenzi mazuri Vengu sasa hivi ana hali nzuri vitu vidogo vidogo anajisaidia yeye mwenyewe, hizi habari za uvumi zinakatisha tamaa..“
Kuhusu Afya ya Vengu amesema ni mzima ila kutokana na ushauri wa daktari anatakiwa awe kwenye utulivu ambao unamfanya awe nje ya kundi lakini yeye bado ni mfanyakazi na anaendelea kulipwa kama kawaida.
“Vengu sasa hivi ana mwaka mmoja na nusu yuko nyumbani kama anaenda Hospitali ni binadamu.. labda Malaria, au labda kichwa kitamuuma ndio tutasema twende Hospitali lakini sio mgonjwa na Komedi wanajua kwamba amepumzika na wao wamekubali kwamba apumzike ili baadae arudi..“
“Madaktari wake ni wakali mno kuna daktari wake hataki suala la kufanya mahojiano au kumkumbusha kumbusha vitu vya nyuma inakuwa kama unamtia huzuni.. kumpa simu asikilize ni vitu ambavyo vimekatazwa“
Msanii wa vichekesho Kitale amezungumzia movie ambayo alikuwa amefanya na marehemu Sharo milionea lakini haikuweza kutoka baada ya kutokea kifo chake, kazi waliyoifanya kwa lengo la kuleta mabadiliko na iwe mfano movie iliyokuwa itoke Desemba 2012, lakini baada ya kuona hakuna mabadiliko kama walivyotegemea ameamua kuitoa ili watu wajifunze ambapo anategemea kuitoa mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment