Rubani Andreas Lubitz
Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.
Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege.
Bwana Robin amesema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.
Hatahivyo abiria walisikika wakipiga nduru kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo,aliongezea.
Rubani huyo kwa jina Andreas Lubtiz,mwenye umri wa miaka 28, alikuwa hai hadi wakati ndege hiyo ilipoanguka ,kiongozi wa mashtaka alisema.
Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliokuwa ikitoka Barcelona kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na kuwauwa abiria wote 144 pamoja na wafanyikazi sita wa ndege baada ya kushuka kwa dakika nane.
"Tunasikia rubani akimuuliza rubani mwenza kuchukua udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vilevile tunasikia sauti ya kiti kikisonga nyuma na mlio wa mlango ukifungwa,bwana Robin aliwaeleza wanahabari.
Mabaki ya ndege ya ujerumani ilioanguka katika mlima Alps na kuua watu150
Aidha polisi nchini Ujerumani wamegundua kile wanachosema kitawasaidia katika kubaini kiini cha rubani msaidizi Andreas Lubitz, kuangusha ndege na kuwauwa abiria wote 150.
Hayo ni baada ya kufanya msako katika nyumba yake.
Polisi hawajatoa taarifa zaidi kuhusiana na kile walichokipata, lakini baadhi ya vitu vyake vikiwemo Kompyuta, vimechukuliwa ili kuchunguzwa.
Huku uchunguzi huo ukiendelea, imebainika kuwa rubani huyo alitatiza kwa muda, mafunzo yake ya urubani mwaka 2008, kutokana na kutibiwa matatizo ya kiakili
Waziri wa maswala ya ndani nchini Ujerumani, Tomas de Maiziere, anasema kuwa, uchunguzi wa kiusalama dhidi ya rubani huyo, haujasema lolote huku, muajiri wake kampuni ya Lufthansa, ikisizitiza kuwa Lubitz alikuwa asilimia mia kuendesha ndege.
Maafisa upelelezi wakiwa katika harakati za uchunguzi
Aidha viongozi wa mashtaka nchini Ujerumani wanasema kuwa wamepata ushahidi unaosema kwamba rubani wa ndege ya Ujerumani ilioanguka katika milima ya ALPS na kuwaua abiria 150 alikuwa amemficha mwajiri wake kuhusu ugonjwa anaougua.
Maafisa hao pia wamesema kuwa walipata kijikaratasi cha ugonjwa kilichokuwa kimekatwa ambacho kilimtaka rubani huyo kupumzika siku ya kuanguka kwa ndege hiyo.
Hatahivyo hawakupata ujumbe wowote wa rubani huyo kutaka kujitoa uhai wake.
Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimeripoti kwamba faili ya rubani Andreas Lubitz mwenye umri wa miaka 27 katika shirika la anga za juu imeonyesha kuwa Andreas alikuwa na matatizo ya akili na alitakiwa kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara.
Ripoti nyengine ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa alilazimika kuchukua likizo ya miezi sita kutoka kwa mafunzo ya urubani kutokana na shinikizo la akili.
No comments:
Post a Comment