Kijana mmoja nchini Ghana huenda akakatwa
kidole chake baada ya pete aliyoiokota na kuivaa kung’ang’ania kwenye
kidole ambacho kimeshaanza kupuputika huku nyama zikianza kuliwa
kimaajabu na kuanza kumtia hofu kijana huyo.
Kijana huyo aliyefahamika kama Eric Buageng, alisema
iliiokota pete hiyo pembeni ya barabara wakati akirudi nyumbani
akitokea Kanisani na kuivaa kwenye kidole cha shahada mkono wa kulia,
lakini cha kushangaza baada ya kufika nyumbani alianza kusikia maumivu
kutokana na pete hiyo kumbana kidole.
Eric amesema
kilichomshangaza zaidi ni wakati alipokuwa anaiokota mkono wake ulikuwa
ukitetemeka na alipojaribu kuitupa hakuweza na kusikia sauti ambayo
hakujua ilipotokea ikimwambia aende nyumbani, alipofika alijaribu kuitoa
lakini hakuweza na kuna wakati anakisikia sauti ikumuamuru atoke nje
lakini haoni mtu yeyote.
Tangu wakati huo jitihada za kujaribu
kuitoa pete hiyo zimeshindikana pamoja na kwenda kwenye Hospitali
mbalimbali ikiwemo ya wataalam wa Jeshi ya 37’ Military na ile ya Korle
Bu Teaching bila mafanikio, katika jitohada za kuhakikisha inatoka
alikutana na wachungaji mbalimbali waliomuombea lakini hakufanikiwa
kuitoa.
No comments:
Post a Comment