TTCL

EQUITY

Monday, March 2, 2015

JE?..UNAJUA KUWA UZITO WA MWILI, KITAMBI NA UNENE VYAWEZA KUATHIRI KWENYE MAHUSIANO YAKO NA HASA TENDO LA NDOA!!?

Asikudanganye mtu bwana, uzito mkubwa wa mwili, kitambi na unene vimewanyima wengi sana kuyafurahia mahusiano yao.

Najua mara nyingine ni ngumu sana kuwa muwazi kwa mpenzi wako kuhusu uzito wake, unene wake au kitambi chake, na unaona utata kumwambia apungue, lakini hiyo haipunguzi ukweli kwamba haufurahii na unajisikia vibaya, na zaidi ni kwamba unatamani sana apungue.

Wala hauhitahi kushurutishwa sana kupungua, faida sio tu kwa mpenzi wako bali kwako pia.

Na kama yeye ndicho anachokitamani, inakuwia ngumu nini ku "sacrifice" kwa ajili yake? kwanini kuamua kupungua isiwe zawadi kwake?

Najua kuna ugumu, na kuna kujitoa kwa dhati lakini uzuri ni kwamba kujitoa huku kunalipa kwako binafsi na kwa mahusiano yako kwa ujumla.

Usije ukanukuu vibaya, Kunatofauti ya unene na makalio makubwa.

Utafiti:Wanaume wanapenda wanawake wenye makalio makubwa 

 

Katika majarida mengi umewaona wanaume wakikodolea macho picha za wanawake wenye makalio makubwa iwe ni kim Kardashian, Jenipher Lopez Nicki Minaj na Vera Sidika kutoka Kenya .
Sasa basi Utafiti umedhibitisha kuwa ni kweli wanaume wanapenda wanawake waliojaaliwa sehemu ya nyuma.

Kulingana na utafiti wa chuo kikuu Bilkent , chuo kikuu cha Texas, na chuo kikuu cha American University kilichoko mjini Beirut
Wanaume wanakisia kuwa mwanamke mwenye makalio makubwa anaweza kufanya kazi kwa bidii zaidi ya mwanamke ambaye hana makalio makubwa.

Hata hivyo kinachowavutia wanaume si makalio haswa bali ni kupinda kwa uti wa mgongo unaosababisha tako kuonekana zaidi.

No comments:

Post a Comment