Baada ya kucheza mechi 22 mfululizo bila kupoteza mchezo wowote, hatimaye wiki iliyopita rekodi hiyo ya Real Madrid ilifikia tamati baada ya kufungwa 2-1 na klabu yaValencia katika ligi kuu ya Hispania.
Pamoja na rekodi hiyo kuvunjwa, Real Madrid bado wana rekodi nyingine ya kuilinda mwishoni mwa juma hili watakapocheza mchezo wao kwanza kwenye dimba la Santiago Bernabeu ndani ya mwaka 2015 dhidi ya Espanyol.
Madrid ambao jana walipoteza mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 bora ya Copa Del Rey dhidi ya Atletico jumamosi hii wanakutana na timu ambayo wamekuwa wakipata matokeo chanya katika misimu mingi ya hivi karibuni.
Mara ya mwisho Espanyol kumfunga Madrid ilikuwa miaka 19 iliyopita katika msimu wa 1995/96, tangu wakati huo Madrid haijapoteza mchezo katika michezo 18 waliyokutana na klabu hiyo ya jimbo la Catalunya.
Katika mechi 18 zilizopita Madrid wameshinda mara 15 na kutoa sare 3 dhidi ya Espanyol.
No comments:
Post a Comment