UDHALILISHAJI WA MAVAZI YA AKINADADA WALETA SURA MPYA KENYA
Angalia hapa chini video ya yule mwanamke aliyevuliwa nguo hadharani baada ya kuvaa nusu uchi huko Kenya.
Kenya Kimenuka kwa Wanawake Wanaovaa Nguo Fupi ama Suruali za Kubana na Kuachia Makalio, Mpaka sasa yameripotiwa matukio kadhaa ya wanawake waliovaa min Skirts kushambuliwa na kuvuliwa nguo hadharani mbele za watu.
Kufuatia umbo la kali na nguo yake yenye kuonesha maungo yake wananchi walishindwa kujizuia na wakatamani kuona kila kitu.
Maandamano hayo yamefanyika chini ya kauli mbiu 'My dress my choice'
Wanawake mjini Nairobi, Kenya leo wameandamana kupinga kitendo cha mwanamke mmoja kuvuliwa nguo wiki jana kwa madai kuwa alikuwa amevalia sketi fupi sana.
Wanawake wengi walikerwa na kitendo hicho wakisema kuwa kila mwanamke ana haki ya kuvalia mavazi yanayomfurahisha.
Hiyo wiki jana kanda ya video ilisambazwa kwa mitandao ya kijamii ikionyesha mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina hadi sasa akivuliwa nguo zake na wanaume katika kituo cha magari ya abiria kati kati mwa Nairobi.
Na wanaume walikuwepo kuwaunga mkono wanawake katika maandamano yao
Wanawake mashuhuri wakiwemo wasanii, wanasiasa na wanaharakati walilaani kitendo hicho wakihoji kwani mavazi ya mwanamke yanamhusu nini mwanamume ambaye sio mumewe wala jamaa yake.
Baadhi walikitaja kitendo hicho kuwa cha kinyama na kinachokiuka haki za wanawake.
Msanii mmoja mashuhuri Nyota Ndogo alinukuliwa akisema ikiwa wanaume wanawavua nguo wanawake kwa kile wanachosema ni mavazi yasiyo ya kiheshima, basi na wanaume wanaolegeza long'i zao na wao basi pia wavuliwe nguzo zao.
No comments:
Post a Comment