Kama macho yako hayakosi Magazeti ya kila siku au kusoma mitandao mbalimbali ni lazima utakua umekutana na stori kwamba Wema Sepetu na Diamond Platnumz wameachana.
Diamond Platnumz alihojiwa kwenye XXL ya CloudsFM November 21 2014 lakini hakuweka wazi kabisa nini kinaendelea lakini maelezo yake yanaweza yakawa na ishara ya jibu linakoelekea.
Moja kati ya alivyovisema ni kwamba hata yeye alishangaa kuhusu ile zawadi ya gari aina ya BMW aliyozawadiwa Wema kwenye birthday yake huku meneja wake Martin akikaririwa na vyombo vya habari kwamba ni marafiki walijichanga kumnunulia Wema.
Baada ya hayo kuna baadhi ya stori zimekua zikitambaa kwamba Martin Kadinda ndio amehusika kuwaachanisha Diamond na Wema Sepetu ambapo aliamua kujibu kwa kuandika hivi kwenye instagram >>> ‘Siwezagi kujibizana.. Ila i gat people who can do that…. Namleta kwenu bingwa wa kutusi watu… Mimi nimemwachanisha wema na chibu ahahahahahaa ahahhahahaha ahahahahaha walaaahi naona raha.. We Nasri that powerful couple ambayo haijawahi kutokea tz na haitakuja kutokea iachanishwe na mimi fundi makoti?? Team kadinda mpeni what he deserve…..’
No comments:
Post a Comment