TTCL

EQUITY

Sunday, November 23, 2014

CHANZO CHA KAMATI YA ZITTO KUGEUKA JUU YA SAKATA LA ESCROW AKAUNT,YADAIWA NI ZITTO KABWE NA KAFULILA KUTAKA ONGO ZAIDI ONA MGAO WALIOPATA AWALI

WAKATI umma ukisubiri kutolewa kwa taarifa ya uchunguzi kuhusiana na akaunti ya Escrow na Bunge, mambo yamezidi kuwekwa wazi ikiwemo madai ya rushwa yaliyokuwa yakitakwa kufanywa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa kampuni ya Independet Power Limited (IPTL).
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya bunge na ofisi za IPTL, zilieleza kuwa kabla ya mjadala huo kupamba moto kulikuwepo na msukumo mkubwa wa kuomba fedha ikiwemo kwa baadhi ya wajumbe wa PAC, akiwemo Mwenyekiti Zitto Kabwe kuwatambulisha watu wake kwa uongozi wa kampuni ya Independet Power Limited (IPTL).
Gazeti hili ilipata nyaraka mbalimbali zilizomuonyesha wakili wa Zitto, Alberto Msando akichukua fedha kwa niaba ya mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini ambaye alimtambulishwa kwa Mwenyekiti Mtendaji wa  PAP, Harbinder Sethi kama mshauri wake wa sheria, baada ya kikao kirefu alichokifanya na mmiliki huyo wa IPTL kabla hajasafiri kwenda India.
Nyaraka za malipo, ambazo gazeti hili ilizipata ambazo zinamuhusisha mtumishi wa bunge, Beatus Malima ambaye ni mmoja wa makatibu wa kamati ya PAC, Malima na wakili wa Zitto, Msando, ambao walichukua milioni 10 kila mmoja kwa nyakati tofauti na kuzipeleka kwa wajumbe  PAC ili waandae Ripoti itakayoonyesha kwamba kwenye IPTL haina Tatizo.
Katika vocha ya malipo iliyotoka PAP inamuonyesha April 8, 2014 Wakili Msando alipokea sh. milioni 10 kwa ajili PAC na Zitto kuandaa majibu ya malalamiko ya kampuni ya MECHMAR dhidi ya IPTL/PAP kazi ambayo inasemekana zitto aliifanya Machi 28, mwaka huu.
Taarifa zaidi zinaonyesha kwamba tarehe hiyo, mtumishi wa bunge anayefanya kazi na Kamati ya PAC, Malima naye alichukua kiasi kama hicho cha fedha kwa kazi hiyo hiyo na baadae Msando alikwenda PAP kuchukua dola 5000 kwa uongozi wa kampuni hiyo.
Gazeti hili ilibaini kuwa pia kampuni hiyo ilimpa Vivian milioni sita, Machi 28, mwaka huu, ambapo baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo, waliokosa fedha wamesema kuna mengi yanayofanywa na PAC, ambao umma unapaswa kujua na tumedhamiria.
“Tumechoka kutumiwa huku wengine wakifaidika na kinachotuumiza zaidi wanasema uongo, wanataka kumuaribia nchi tu, Rais Jakaya Kikwete kwa kila wakati kuhakikisha anabadilisha baraza la mawaziri kwa shutuma za uongo na za kupikwa,”alisema mbunge mmoja
Alisema sasa tutaeleza ukweli kwa kuwa kuna watumishi wa bunge walikuwa wanatumwa kwenda kuchukua fedha na kilipotakiwa kiasi cha bilioni 1.5 ili kuzima mjadala ndipo haya mambo yameibuka kwa kuwa  IPTL waligoma kutoa fedha.
“Sisi ni wanasiasa lazima tuwe wakweli katika kila tunachokisema au kukisimamia kwa kuwa tukiacha hivihivi, hatutafika tunapopataka zaidi kwa kuwa PAP waliipata IPTL kwa kufuata taratibu zote kisheria pamoja na malipo waliyopewa katika akaunti ya Escrow yalikuwa halali kwao ila hila za watu ndio wanaosababisha haya yote,”alisema mbunge huyo.
IPTL iligoma kutoa fedha kwa baadhi ya wajumbe wa PAC, pale walipotaka walipwe kiasi cha billioni 1.5 ili wazuie mjadala uliotarajia kuibuliwa kipindi hicho kuhusu sakata hilo, ambalo kunadaiwa kuna kundi kubwa la wafanyabiashara nyuma wakifanya haya.
Hivyo, alisema wabunge wengi wamejiandaa kueleza ukweli ndani ya bunge pamoja na kutoa mawasiliano ya simu kati ya wajumbe wa PAC na baadhi ya wabunge kuwaomba wawape nguvu katika suala hilo, pamoja na mawasiliano ya fedha kwa viongozi wa PAP yalivyokuwa yakifanyika.

No comments:

Post a Comment