Bwana harusi mmoja kutoka Saudi Arabia amempa talaka mkewe siku ya harusi baada ya kumuona uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha alipotaka kuwapiga picha.
Maharusi hao kutoka mji wa magharibi wa Saudia,Medinah walikubaliana kuoana licha ya kutoonana uso kwa uso,swala ambalo ni utamaduni mkubwa wa mataifa ya mashariki ya kati.
lakini wakati mwanamke huyo alipofungua kitambara alichokuwa amejifunika uso na kutabasamu katika kamera,mumewe alishtuka na kuondoka wa ghafla.
Kulingana na gazeti moja katika eneo hilo kwa jina Okaz,mwanamume huyo alianguka na kuzirai huku wageni waalikwa wakijaribu kuingilia kati ili kutatua kilichokuwa kikiendelea.
Hatahivyo Bwana harusi alisema kuwa hakuweza kumwona bi harusi kabla ya harusi yao gazeti hilo la Okaz liliripoti.
'' Si wewe msichana niliyetaka kuoa,si wewe kamwe niliyedhani '' kwa hivyo nakupa talaka''alisema bwana harusi.
Na alipompa talaka bi harusi naye alianguka na kuzirai na kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa majonzi.
No comments:
Post a Comment