Kwa
kawaida mashabiki wa mpira wa miguu, mpira mikono, mpira wa kikapu au
hata ‘handball’ huingia kwa wingi uwanjani kushangilia mechi kati ya
timu zao na wapinzani. Lakini hii imekuwa tofauti kwa mashabiki wa mpira
wa Volleyball huko Taiwan.
Vyombo
vya habari vya nchini humo vimeeleza kuwa wadau wa mpira wa Volleyball
wamemlalamikia mchezaji wa kike mrembo na mwenye mvuto haswaa
anaefahamika kwa jina la Sabina Altynbekova kuwa chanzo cha kuharibu
uhalisia na utamu wa mechi za mchezo huo pale timu yake inayoitwa
‘Kazakhstan’ inapokutana na timu nyingine.
Taarifa
hizo zinaeleza kuwa umati wa mashabiki hasa wanaume wanaonekana kuwa
huingia uwanjani kumuangalia zaidi msichana huyo mwenye umri wa miaka
kati ya 17 na 18, na hivyo mvuto wake huharibu uhalisia wa mechi kwa
kuwa kila anaposhika mpira hushangiliwa sana kama ndiye mchezaji pekee
kitu ambacho kinaonekana kuwa tatizo hata kwa wachezaji wenzake.
Kocha
wa timu hiyo, Nurlan Sadikov pia ameonekana kusikitishwa na hali hiyo
inayoathiri saikolojia ya wachezaji wengine wa timu yake.
“Haiwezekani
ifanyike hivi…umati wa watu unafanya kama vile kuna mchezaji mmoja tu
kwenye hii ligi hii ya mabingwa.” Kocha Sadikov aliiambia Tengrin News.
No comments:
Post a Comment