KATIKA ulimwengu wa mastaa wa
Kibongo, kuna vijimambo kibao mojawapo ni wale wa kike kujiingiza kwenye
mapenzi na kudanganywa kilaini kisha kushiriki mchezo wa kikubwa bila
usalama (kinga).
Matokeo yake ni kuzalishwa na kuachwa solemba na sasa wanalea
watoto wao wenyewe bila baba zao.
Unajua sababu? Ni ileile, yaani kupenda maisha ya ghali wakati hawana
uwezo hivyo kujikuta wakijinasua kwa kujirahisisha kimapenzi kwa
wanaume.
Leo Ijumaa Wikienda linakuletea mastaa 10 wa Kibongo waliozalishwa na kuachwa solemba wakilea watoto bila baba zao.
Alianzia kwenye filamu kisha
akajiingiza kwenye muziki. Kwa mujibu wake mwenyewe, aliwahi kukiri kuwa
aliingia kwenye fani hizo kwa ajili ya kujitafutia kipato ili kulea
wanaye. Aliolewa ndoa ya kwanza huko kwao Tabora na kuzalishwa mtoto
mmoja kisha ndoa ikaota mbawa. Hakukaa muda mrefu akapata mwanaume
mwingine ambaye alimpa ujauzito na kuzaa mtoto wa pili. Aliwahi kusema
kati ya wanaume hao, hakuna anayemsaidia kulea.
ISABELLA MPANDA
Alianzia kwenye urembo, akatwaa Taji
la Miss Ruvuma 2006 na sasa anafanya filamu na muziki. Ana watoto wawili
wa kiume ambao amezaa na wanaume tofauti. Anakiri kuwa anamshukuru
Mungu kwa kuwa anaweza kuwapatia malezi bora wanaye kwa msaada kiduchu
kutoka kwa wanaume hao.
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Alianzia kwenye uigizaji kisha urembo
na sasa ameongezea muziki. Amezaa na Mkurugenzi wa Tuesday
Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ ambapo walijaliwa kupata
mtoto mmoja wa kike na baada ya hapo mapenzi yakaisha. Kwa kuwa mapenzi
yalikwisha, Jini Kabula alibaki na mwanaye akimlea mwenyewe japo Mr Chuz
huwa anampiga ‘tafu’.
JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’
Alianzia kwenye urembo kisha akaingia
kwenye filamu na muziki. Ana mtoto mmoja. Anakiri kuwa mtoto huyo
alizaa na mwanaume mmoja ambaye hakumtaja kwa jina lakini baada ya hapo
waliachana na anaendea kumlea mwanaye peke yake.
NURU NASSORO ‘NORA’
Mwigizaji huyo aliolewa na mwanaume
wake wa kwanza ambaye alimzalisha mtoto mmoja wa kiume. Baadaye
waliachana na kuanzia hapo hakumsaidia chochote kuhusu matumizi ya mtoto
hadi mwanaume huyo alipofariki dunia na sasa anamlea mwanaye mwenyewe.
JACQUELINE DUNSTAN ‘JACK WA MAISHA PLUS’
Alipata umaarufu kupitia Shindano la
Maisha Plus II kabla ya kujiingiza kwenye filamu. Aliachwa solemba baada
ya kuzalishwa na mwanaume ambaye hadi sasa hana mawasiliano naye na
hajui alipo hivyo analea mwanaye mwenyewe akiwa kwa bibi yake mkoani
Morogoro.
SNURA MUSHI
Alianzia kwenye uigizaji kabla ya
hivi karibuni kujikita pia katika tasnia ya filamu. Ana mtoto mmoja wa
kike. Anakiri kuwa tangu akiwa mjamzito baba mtoto wake aliingia mitini.
Mpaka sasa anamlea mwanaye mwenyewe kupitia sanaa ya filamu na muziki.
FAIDHA OMARI ‘SISTER FAY’
Japo hasikiki sana, mwanzoni
alijikita kwenye muziki na hivi karibuni ameongezea nyingine ya
uigizaji. Ana mtoto mmoja aliyejifungua mwaka jana. Anakiri kuachwa njia
panda na mwanaume aliyemzalisha kwani hadi sasa anamlea mwanaye
mwenyewe.
MAUNDA ZORRO
Alipata umaarufu kupitia muziki na
baadaye akaongezea uigizaji. Ana mtoto mmoja na huwa hapendi kumwanika
mwanaume aliyemzalisha ambapo mpaka sasa anaishi nyumbani kwa baba yake,
mzee Zahir Zorro na hakuna dalili zozote za ndoa.
YVONNE-CHERRY NGATIKWA ‘MONALISA’
Mwigizaji huyu legendary pia ni
Mtangazaji wa Radio Times FM. Alijaliwa kupata mtoto na prodyuza wa
filamu za Kibongo, George Otieno ‘Tyson’ ambaye alikuwa ni mume wake wa
ndoa. Baadaye waliachana akaolewa tena kwa ndoa ya Kiislam na kupata
mtoto mwingine. Mpaka sasa anaishi na watoto wake na anawalea kupitia
kazi zake za filamu na utangazaji.
No comments:
Post a Comment