TTCL

EQUITY

Saturday, January 4, 2014

MHUBIRI AFA MAJI BAADA YA KUJARIBU KUTEMBEA JUU YA MAJI KAMA YESU.

Ilikuwa sikitisho kubwa kwa waumini baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile masihi Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani.


Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.

Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi.

Tukio Hili la kusikitisha limetokea Huko Nigeria.

No comments:

Post a Comment