Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ameirudishia Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya Mkoani
Geita zawadi ya gramu 227 za dhahabu safi akielekeza kuwa zawadi
hiyoitumike kuwasaidia watoto yatima.
Rais Kikwete ametoa
maelekezo hayo leo, Jumatatu, Novemba 11, 2013, baadaya kukabidhiwa
zawadi ya dhahabu hiyo wakati wa sherehe ya kuzindua mgodi wa uchenjuaji
dhahabu wa kampuni hiyo nje kidogo ya mji mdogo wa Kharuma ambako ndiko
makao makuu ya wilaya mpya ya Nyang’hwale,Mkoa wa Geita.
Gramu hizo 227 ambazo ni sawa na aunzi nane zina thamani ya Sh. milioni 16 kwa bei ya sasa ya soko la dhahabu duniani.
Baadaya kukabidhiwa zawadi hiyo, Rais Kikwete ameuliza: “Sasa nifanye
nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii dhahabu, iuzeni popote mnakotaka
na fedha itakayopatikana tutawapa watoto yatima.”
Akizungumzana
wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete ameupongeza uongozi wamgodi huo
akisema kuwa umeongeza thamani ya dhahabu na ya maisha yawananchi
katika eneo hilo nje ya mji mdogo wa Kharuma.
Hatahivyo, Rais
Kikwete ameushauri uongozi wa mgodi huo kufanya jitihada za kuboresha
teknolojia inayotumika. “Mmefanya vizuri sana na mgodi huu ni mradi wa
maana sana kwa kuongeza thamani ya dhahabu na kuboresha maisha ya
wananchi katika eneo hili. Ubunifuhuu unastahili pongezi.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Lakini lazima tuboreshe teknolojia. Teknolojia
inayotumika kwenye mgodi huu bado ni ya zamani kidogo. Hii ni sawa na
hadithi ya mtu mwenye chongo katika jamii ya vipofu watupu. Yeye
anaonekana kama mfalme.”
Mgodi wa Nyamigogo ambao ni mgodi wa
marudio kwa maana ya kwamba unazalishadhahabu kutokana na mchanga ambao
huko nyuma umepata kufuliwa nakutoa dhahabu, ulianzishwa mwaka 2011 na
mpaka sasa zimewekezwa kiasicha Sh.bilioni 1.6 katika uendelezaji wa
mgodi huo.
Risala ya uongozi wa mgodi huo inasema kuwa mgodi
huo unaozalisha kiasi chagramu kati ya 500 na 600 kwa mwezi na unaajiri
watu 45 wakiwemo wanawake 10.
Tokea kuanzishwa kwake, mgodi huo
umekuwa unaunga mkono shughuli za jamii inayouzunguka ikiwa ni pamoja
na kujenga zahanati na madarasa yashule katika vijiji viwili.
Rais Kikwete amezindua mgodi huo ikiwa sehemu ya kukagua na kuzindua
miradi ya maendeleo katika ziara yake rasmi ya kikazi katika Mkoa
waGeita, moja ya mikoa minne ambayo aliianzisha mwaka jana. Mikoa
mingine ni Simiyu, Njombe na Katavi.
Ziara hiyo ya siku tano
inamalizika kesho, Jumanne, Novemba 12, 2013, na mbali ya kuzindua mgodi
huo, Rais Kikwete leo amepokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya
Nyang’hwale na kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kharuma
uliohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi.
Rais kikwete anatarajia kufanya majumuisho ya ziara yake Jioni ya leo!
No comments:
Post a Comment