Askari aliyegongwa na kufa akiwa amefunikwa nguo. |
Askari
wa Usalama balalani jana aligongwa na kufa hapo hapo jana katika
msafala wa Rais J.K, maeneo ya Bamaga, Mmoja kati ya raia walio shuhudia
tukio hilo akielezea hali jinsi ilivyokuwa.
"Ndugu
zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha na
yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua
speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance.
Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:
Alihisi
kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so akawasimamisha mungu saidia
alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. Bila ya kuangalia
nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from Shekilango road na hapo
ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na speed kama
120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna magari
yanayo-cross from Shekilango.
Jinsi
gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC badala
ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala hamadi
traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona sekunde
ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila baada
ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona
nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia
sasa na wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua
si kitu kizuri kutazama.
Ila
nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule mama
nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta.
Binafsi nimechukulia kama fundisho kwangu, sina mtazamo kama wa wachangiaji wengi wa juu yangu."
No comments:
Post a Comment