AFANDE SELE AKIWA NA MBUNGE WA KAWE (CHADEMA), HALIMA MDEE
Rasmi leo msanii maarufu wa hip hop, Afande Sele amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Afande ameonyesha ni mwenye furaha na kwenye mtandao wa Facebook ameweka maneno haya.
Hakuna
kusanda,hakuna kumbwanda,mbele kwa mbele makamanda,vua gamba vaa gwanda
kisha kaza mkanda, wanashuka sisi tunapandaaa,,,,Leo tunaanza kuandika
hisyoria mpya ktk mkoa wetu wa morogoro na tz kwa ujumla kwa sababu
nikiwa kama msanii wa muda mrefu na mfalme pekee wa mzk wa kizazi kipya
ninaetunga nyimbo zangu kwa kuzingatia ujumbe muhimu ktk jamii kwa mambo
ya kisiasa,kiuchumi,elimu,amani na upendo nk,sasa leo nimeamua kwa
ridhaa yangu iliyosukumwa na uzalendo na mapenz makubwa kwa taifa langu
kuchukua kadi ya kujiunga rasmi uanachama wa CHADEMA,tukio hilo kubwa
litafanyika leo jioni ktk mkutano wa hadhara utakaofanyika kata yetu ya
mafiga/misufini na utahudhuriwa na viongoz mbalimbali wa chama kutoka
makao makuu ya chama dsm pamoja na mbunge wa nyamagana mh ezekiel
wenje,kwa wakaz wa moro wazalendo nyote mnakaribishwa saaana,ahsanteni
wana'ndugu,siasa si uadui,tupingane/tusipigane,Pendo moja!
No comments:
Post a Comment