TTCL

EQUITY

Wednesday, October 9, 2013

ROSE NDAUKA; NAPENDA BISKUTI NIKIWA LOCATION

MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Bongo Rose Ndauka amebadilika na kuwa na staili ya kipekee, msanii huyo ambaye ni mahiri katika uigizaji wa filamu amebadili staili yake tofauti na hapo awali watu walivyokuwa wakimjua anapokuwa location, siku hizi inasemekana pamoja na mtayarishaji wa filamu kumlipa mkwanja lakini kuna kitu cha ziada.

Rose akiwa Location kwa sasa hata akipewa mahitaji yake kama ya chakula na vinywaji lazima umnunulie pia maboksi ya Biskuti atakula lakini yeye mara nyingi amekuwa kipenzi cha watoto anaowakuta eneo husika kwani lazima kabla ya kuanza kurekodi ataanza kugawa kwa biskuti kwa watoto kisha kufurahi nao hapo atakuwa tayari kwa kazi.

“Rose Ndauka bwana ukiwa naye location hakikisha unakuwa na maboksi ya biskuti kabisa bila hivyo kazi italala, maana anapotaka vitu vyake apewe bila kuchelewa nimefanya naye kazi hali ilikuwa hivyo, nashukru nimemaliza,”anasema mtayarishaji mmoja.

Lakini awali kuna watu walikuwa wakijiuliza kuwa mara nyingi imekuwa ikiripotiwa kuwa msanii huyo upiga mitungi kiaina sasa watu wa masanga na biskuti wapi na wapi? Kumbe anapotaka biskuti inakuwa ni sadaka kwa watoto ambao yeye anawaona kama marafiki wa kweli.

Soma zaidi: http://mwanahabariuswazi.blogspot.com/2013/09/rose-ndauka-napenda-biskuti-nikiwa.html#ixzz2hFzkJE5a

No comments:

Post a Comment