Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ,
limekanusha taarifa zilizotapakaa kwenye mitandao kuwa askari wa jeshi
hilo waliokwenda huko kwa ajili ya kulinda amani,wameanza kujihusisha na
makahaba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Habari na
Uhusiano, Mtandao wa www.congodrcnews.com wanajeshi wa Tanzania wameanza
kujihusisha na ubakaji wanawake katika Mji wa Sake ulioko Goma.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa askari mmoja wa JWTZ
alihitaji kujamiiana na mwanamke mmoja(Kahaba) kwa ujira wa Dola 50.
Baada ya kumaliza shida zake ambazo ilielezwa alizifanya bila kinga
yoyote,askari huyo alikataa kumlipa ujira wake,hali iliyoleta tafrani na
mwanamke huyo kupiga kelele.
“JWTZ linapenda kuwaeleza wananchi kuwa taarifa
hizo ni za uongo mtupu wenye nia ya kulipaka matope JWTZ na Tanzania kwa
ujumla. “Picha iliyotolewa kwenye tovuti hiyo ya www.congodrcnews.com
ni ya wanajeshi wa Tanzania walipokuwa katika Operesheni ya huko Comoro
mwaka 2008.
Mtu anayeonekana kuwa chini ya Ulinzi alikuwa ni mshiriki wa Kanali Mohamed Bacar ambaye aliondolewa madarakani.
“Vilevile picha hiyo ilitolewa vile vile katika tovuti za www.apc.net.au/news/stories ya Machi 26, 2008 na ww.
Seattletimes.com. na pia picha hiyo ipo pia kwenye
tovuti ya Jamii Forum baada ya kufanya ‘link’ kutoka kwenye Mtando wa
www.google.com.”
Taarifa hiyo ilisema kuwa JWTZ inapenda kueleza
wananchi na dunia kwa ujumla kwamba wanaoneza taarifa hizo wana lengo la
kukatisha tamaa juhudi zinazofanywa na
nchi za Maziwa Makuu na SADC kuleta amani nchini
DRC kwani JWTZ wako DRC kwa mujibu wa taratibu za kiutendaji za Umoja wa
Mataifa.
No comments:
Post a Comment