TTCL

EQUITY

Saturday, November 29, 2014

YANAYOJIRI BUNGENI: HAYA NDIYO MAAZIMIO MAPYA WALIYOKUBALIANA WABUNGE KUHUSU SAKATA LA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW


Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe amesoma maazimio mapya ya Bunge kwa mujibu wa kamati maalumu iliyoundwa leo na kuhusisha CCM, PAC na UKAWA


Azimio: Mamlaka ya uteuzi iwawajibishe na inashauriwa kutengua uteuzi wa Waziri wa Nyumba, ardhi na makazi Prof Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo, Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Werema, na Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Maswi



Azimio: Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge

Azimio: Mamlaka husika ziitangaze Benki ya Stanbic, Mkombozi na benki yoyote nyingine itakayogundulika kuwa zinahusika na utakatishaji wa fedha haramu

Azimio: Kwa kuwa majaji walihusika, Rais aunde Tume ya kijaji ya uchunguzi na kuwasimamisha jaji Mujulusi na Prof Luhangisa



Azimio : Serikali ipitie upya mikataba ya Umeme na itoe taarifa kabla ya kumalizika kwa mkutano ujao wa bunge la Bajeti

Azimio : Serikali ichukue mitambo ya IPTL na iikabidhishe kwa TANESCO
Azimio: TAKUKURU na Polisi wamchukulie hatua bwana Sethi, na kumfungulia mashitaka akithibitika


Wasira: Tuamini kwamba haya yote ni kwa maslahi ya watanzania, CCM imeshirikiana na kambi ya upinzani kufanya maamuzi sahihi
Spika awahoji wabunge, na wao wamepitisha azimio la bunge kama lilivyosomwa na @zittokabwe

No comments:

Post a Comment