TTCL

EQUITY

Saturday, October 18, 2014

Kutoka Escape 1 huyu ndiye mshindi wa Serengeti Super Nyota 2014.

40dv
Mashindano ambayo yalikusanya jumla ya wasichana 14 kutoka miji 14 tofauti kwa ajili ya kutafuta kipaji kimoja ambacho kitawakilisha hiyo miji mingine hatimaye kimepatikana usiku wa kuamkia October 18 pale Escape 1.

Meza ya majaji 4 wakiongozwa na Dj Fetty walikua na kazi ya kuhakikisha wanapata kipaji kimoja ambacho mbali na kupewa zawadi ya Milion 1 taslim pia atapata nafasi ya kupiga colabo na Diamond Platnumz na darasa la muziki kutoka kwa Barnaba.
Hellen George ndiye aliyepata nafasi hii kwa kuibuka mshindi wa mashindano haya kwa mwaka huu ambaye anawakilisha mkoa wa Dar es salaam,mara baada ya kutangazwa mshindi,millardayo.com ilipata nafasi ya kufanya nae interview fupi juu ya ushindi huo.

30dv
Hellen George mshindi wa Serengeti Fiesta Super Nyota 2014.

‘Namshukuru Mungu kwa hii nafasi na nafurahi kwa kamati iliyoandaa shindano hili kwani imelenga kuinua vipaji vyetu,kiukweli shindano lilikua gumu na lilikua linahitaji moyo,nimejisikia furaha kutangazwa mshindi’
‘Mshiriki niliyekuwa namuangalia zaidi ni mshiriki kutoka Mwanza sio kwamba nilikuwa namhofia lakini nilimgundua ana kitu tofauti kwenye sauti yake,nafasi hii nimeifurahia kwa sababu Diamond Platnumz ni msanii ambaye nampenda sana,nilishawahi rekodi single 1 mpaka sasa lakini haikwenda radio’-Hellen George.

39dv
33dv
27dv
25dv
17dv
Hawa ndiyo 3 bora wa kwanza kushoto ni Siamary Tarimo kutoka Moshi,katikati Mshindi Hellen George wa Dsm na mshindi wa tatu Halima Ramadhan kutoka Dodoma.

11dv
6dv
1dv
5dv
3dv
20dv

No comments:

Post a Comment