Madaktari
Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter
Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya
nchini India wakimwekea mgonjwa kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme
kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital
kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma
mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).
Madaktari
Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter
Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya
nchini India wakimwekea mgonjwa betri ambalo litatumiwa na kifaa
kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI
kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab
wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila
kufungua kifua (Catheterization).
Daktari
bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge
akimuhudumia Monica Mahenge ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo baada ya
kufanyiwa matibabu ya moyo kupitia mishipa ya damu bila kufungua kifua
(Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab . Monica ni mmoja kati
ya wagonjwa 16 ambao JKCI kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Hospitali
ya BLK ya nchini India walitoa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya
moyo (Valve), balloon mitral valve procedure (Valvuloplasty), kuzibua
mishipa ya damu ya moyo, kufunga kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme
(Pacemaker) na kuangalia utendaji kazi wa Moyo.
Madaktari
bingwa wa Moyo, Wauguzi, Technologists, wataalam wa dawa za usingizi
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kumpatia mgonjwa
huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve) bila kufungua
kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab .
Kazi
ya kutoa huduma ya matibabu ya Moyo kwa mgonjwa kupitia mishipa ya damu
bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab
ikiendelea.
No comments:
Post a Comment