Ni mrembo, Model, Fashionista, Actress,Video queen, na Mama huyu ni HAMISA MOBETO, I dont know how she does all this but she
surely does it with style, Hamisa ni mama wa mtoto mmoja sasa but figure yake imerudi
kuwa kama zamani sijui alifanya diet au ni maumbile tu maana wengine
mungu kawajaalia na neema hiyo ya kujifungua na kurudia shape zao bila
mazoezi au diets.
Hamisa kwa insta page yake utakutana na
picha zake nyingi akiwa kapigilia mikato mikali iwe ni otds au otn yeye
huwa anapendeza siku zote.
Hata dish dash hizi anavaa na anapendezaa
Kikazi zaidi aki model vivazi vya Amina design
Anatoka kihivi ndani ya skinny jeans
Vitenge pia huvaa na kumwonesha mrembo sana
Throwback kidogo ya Martenity styles zake hizi tuli-post hapa hata kipindi ana mimba alikuwa anapendeza hakujiachia kidogo kama hivi.
Hamisa Hassani Mobeto amezaliwa mwaka 1994 mkoani Mwanza na kabila lake
ni Mnyamwezi. Mwanzo wake katika tasnia ya u-miss na modelling ilianza
baada ya hamisa kuibuka mshindi wa shindano la Miss XXL BACK TO SCHOOL
BASH Mwaka 2010 iliyoandaliwa na kipindi cha XXL kutoka Clouds Fm.
Mwaka 2011 Hamisa alishiriki mashindano ya Miss Dar Indian Ocean na
alifanikiwa kushika nafasi ya pili , pia mwaka huohuo alikua mshindi wa
pili wa miss kinondoni na kufanikiwa kuingia kwenye Nusu fainali ya miss
Tanzania.
Hapa ni katika kivazi cha mtoko na kimemtoa sana, ukimkuta njiani lazima uzubae |
No comments:
Post a Comment