Makala hii inachambua kwa kifupi jinsi ya kuwa mbunifu. Haijalishi ubunifu ni wa namna gani - iwe kuandika kitabu, kuzalisha vyakula, kutoa huduma za ufundi n.k , yote hayo yanaweza kufanyika kwa ubunifu na kuleta manufaa.
Zingatia hatua zifuatazo:-
1.
Jifunze kulikubali tatizo kama changamoto na fursa ya kuleta suluhisho:
Wapo wengi ambao wanapoona ugumu katika jambo fulani, wanasita kuendelea au
wanasubiri suluhisho toka kwa wengine. Ni kweli kuna mambo utawaachia wengine, lakini
lile 'lililo karibu' na uwezo wako waweza litatua. Mfano ukaribu ninaozungumzia
hapa inawezekana ni mazingira unayoishi, aina ya ujuzi wako, na uwezo wako
2.
Tumia muda wa kutosha kujifunza: Ili kuwa mbunifu
inakupasa uwe na taarifa za kutosha kuhusu tatizo unalotaka kutatua, ujue pia
wengine wamefanya nini. Kujifunza ndio kunakopelekea uzoefu, na uzoefu au
kubobea katika kitu ndiko kunakoleta ubunifu. Kumbuka kujifunza sio lazima
uende darasani, waweza jifunza kwa kuona, kusikia, kujisomea, au kwa
kufundishwa-darasani au sehemu nyingine yoyote ile.
"Ubunifu
ni namna tuu ya kuunganisha vitu. Ukiwauliza watu wabunifu waliwezaje kufikia
walivyofanya, wanajisikia hatia kwakuwa kiukweli hawakufanya lolote, bali
waliona tuu kitu fulani. Ilionekana wazi kwao baada ya muda fulani. Hiyo ni kwa
sababu waliweza kuunganisha uzoefu waliokuwa nao, na kuweka vitu kwa pamoja.Na
sababu ya wao kuweza kufanya hivyo ni kuwa walikuwa na uzoefu, au walitumia
muda mwingi zaidi kufikiria kuliko watu wengine, kuhusu uzoefu wao".
3.
Thubutu Kuota: Baada ya kulitambua tatizo, ukawa
tayari kulitatu, ukajawa na hamasa ya kujifunza, na ukajifunza vya kutosha
kuhusu hali husika, kinachofuata ni wewe sasa kufikiria suluhu ya tatizo
husika. Unachopasa sasa ni kupendekeza njia tofauti ya kufanya jambo, aina mpya
ya bidhaa au huduma, na kujaribu hicho unachofikiria ili kilete mafanikio.
Katika hali hii, Usiogope kukosea, na wala usiogope kuwa kitu chako
kitakataliwa au kuonekana cha ajabu mbele ya watu wengine. Kwani kiuhalisi, ni
kweli ni kitu tofauti hivyo jinsi watu wengine watakavyokipokea itakuwa
tofauti.
Kuwa
mbunifu sasa..!!!
No comments:
Post a Comment