Ni
safari ambayo wameianza August 13 mwaka jana (2012) lakini haijafikia
hapa bila matatizo, wanakwambia Bajaji imezingua sana kwenye baadhi ya
nchi na kuna wakati injini ilisumbua wakajua ndio mwisho wa safari mpaka
wakati mwingine wanalazimika kushuka na kuanza kuivuta wao wenyewe.
Unaambiwa
hii rekodi itaingia kwenye kitabu cha Guiness kama watamaliza safari
yao ambayo wamepanga kuimalizia Brazil kabla ya December 23 2013 kisha
kurudi zao nyumbani Uingereza.
Wanasema
wengine wameshindwa kuamini kama wanaizunguka dunia kwa ‘tuktuk’ a.k.a
Bajaji ambapo kwenye mpaka wa Kenya na Uganda walisimamishwa na Polisi
ambae aliwaambia haamini kuhusu urefu wa safari yao ila kama ni kweli,
itakua ngumu wao kupata watoto wa kiume.. labda wa kike.
No comments:
Post a Comment