Mwanamke wa India mwenye miaka 24 amelazimishwa kuolewa na
kubakwa na kundi la wanaume kama adhabu ya 'heshima' baada ya kaka yake
kutoroka na rafiki yake wa kike, imebainika jana.
Mwanamke huyo - ambaye hakuweza kutajwa kwa usalama wake -
aliambiwa anatakiwa kuolewa na mume ambaye ni kaka wa mke wa mchumba mpya wa
kaka yake kama 'kisasi' kwa uzinzi wa wawili hao.
Na ndani ya masaa kadhaa za kufunga pingu za maisha na
mumewe mpya, akashambuliwa na kubakwa 'bila huruma' na kaka kadhaa wa mchumba
wa kaka yake.
Kwa namna ya kushangaza, shambulio hilo ya kutisha lilidaiwa
hata kupewa kibali na wazee wa kijiji hicho kilichopo makazi ya vijijini ya
Uttar Pradesh, kaskazini mwa India, ambao walidai: "Jicho kwa jicho ni
hukumu halisi."
"Ninakubaliana na uamuzi wao sababu ninajua kwamba
kungekuwa na umwagaji damu katika kijiji hiki kama ningekataa kuolewa
naye," mwanamke huyo aliwaeleza polisi.
"Mashemeji zangu walinibaka bila huruma siku hiyo hiyo
niliyofunga ndoa. Ikawa utaratibu wa kawaida.
"Baba mkwe wangu alidai kwamba amekubaliana na ndoa
yangu kwa vile alitaka kulipa kisasi (kwa familia yangu) namna hii."
Ajali hiyo mbaya imekuja kujulikana tu pale muathirika
alipopata ujasiri wa kufungua madai hayo polisi.
"Machi 26, walifungua kesi dhidi ya kaka yangu na
polisi walimkamata yeye na (mke wa mume wangu). Waliachiwa baada ya binti huyo
kukiri mbele ya hakimu kwamba aliolewa naye kwa hiari yake," muathirika
huyo alidai kwenye madai yake.
Baraza la kijiji au Panchayat, lilidaiwa kumlazimisha
mwanamke huyo kuolewa baada ya kaka yake kuwa ametoroka na dada wa mumewe
mtarajiwa mnamo Februari 15, mwaka huu.
Panchayat, ambalo liliketi ndai ya siku kumi baada ya
kutokomea huko, lilitaka ndoa ya lazima. Mbali na hili, pia liliwataka wazazi
wa mwanamke huyo kulipa Rupia 75,000 kama fidia kwa wakwe zake wapya.
Panchayat baadaye lilifafanua hali hiyo iliyojitokeza,
likisema 'jicho kwa jicho ni hukumu halisi'.
Watuhumiwa hao wa ubakaji - wanafamilia wanaoshitakiwa
-waliripotiwa kuweka bayana kwamba ilikuwa ni ulipizaji wao kisasi kwa kitendo
cha utoroshwaji.
Mwanamke huyo kwa namna fulani alifanikiwa kukwepa majaribio
yao ya kumkamata Julai 21, mapema asubuhi, na kufungua madai kwa polisi wa
Muzaffarnagar mnamo Julai 27.
Mkuu wa polisi, Manzil Saini alisema: "Muathirika huyo
amekutana nami. Kesi imefunguliwa chini ya Kifungu 376 ya IPC. Watuhumiwa
watakamatwa hivi karibuni."
Kaka mkubwa wa muathirika huyo alidai uamuzi huo uliopelekea
tukio hilo ulichukuliwa chini ya usimamizi madhubuti wa Panchayat.
"Polisi walitoa muda kwa watuhumiwa kuondoka kijijini
hapo. Mume huyo wa chifu wa panchayat alikuwapo wakati tukio hilo la dada yangu
likiamuliwa. Alikuwa msemaji mkubwa na kutaka adhabu kali mno dhidi yetu,"
alisema.
Mkuu wa panchayat alithibitisha uamuzi wake jana. Alidai
aliwataka wafikie suluhisho la amani.
Tukio hilo limekuja wiki mbili baada ya mwanachuo mwenye
miaka 20 kubakwa na kundi la wanaume na kisha kuchomwa moto huko Etawah,
jimboni Uttar Pradesh, mkoa alikotokea Waziri Mkuu Akhilesh Yadav.
Katika kesi hiyo, kwa namna ya kushitusha, polisi hao si tu
kwamba mwanzoni walikataa kufungua kesi lakini pia walionekana kukiuka wajibu
wao wa kusimamia sheria na utii.
No comments:
Post a Comment