TTCL

EQUITY

Tuesday, July 12, 2016

Museveni aketi barabarani kupokea simu

 Yoweri Museveni
Bw Museveni alipokea simu kando ya barabara wilaya ya Isingiro, karibu na mpaka wa Uganda na Tanzania 
 
Je ushawahi kupokea simu ya dharura? Je wewe hujitenga vipi na watu waliokaribu nawe ima ni mkeo ama hata wafanyakazi wenza ili upokee simu ya kibinafsi?
Na je katika enzi hizi za simu za kisasa au Smartphone wangapi wetu wanatumia simu za kale zisizo na touchscreen?
Haya basi, Hayo sio maswali ya kipima joto ... la!
Rais wa Uganda Bw Yoweri Kaguta Museveni alizua kioja katika kijiji cha Kyeirumba, wilaya ya Isingiro karibu na mpaka wa Uganda na Tanzania aliposimamisha msafara wake wa magari ili apokee simu "ya dharura". Picha za kisa hicho zilipakiwa kwenye mtandao wa Facebook na afisa wake wa habari Don Wanyama.
Amini usiamini Rais Yoweri Museveni, alishuka kutoka kwenye gari lake rasmi akachukua kiti chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu faraghani.Wenyeji walifurahia kuwa na mgeni ambaye hawakumtarajia   

Museveni
Mzee Museveni kama vile baba wa taifa alitumia muda wake kufanya shughuli hiyo huku akiwapungia mkono wapita njia.

Baada ya dakika 30 hivi raia wa kijiji hicho walishangaa kuwa miongoni mwa maafisa wakuu serikalini.
Ilikuwa ajabu sana kwao kumuona Museveni akiwa ameketi barabarani.
Waganda katika mitandao ya kijamii wamesambaza picha hiyo ya rais museveni akizungumza kwa simu ambayo inaonekana kuwa sio ya kisasa.
Wengine wanamkejeli kwa kuhofia kudukuliwa huku wengine wakimkosoaa kwa kuketi barabarani.
''Kwani hangeweza kupokea simu yake ndani ya gari lake?"
''Ni siri gani hiyo ambayo hakutaka hata walinzi wake wasikie.
''Ama ilikuwa ni #Besigyexit?", wakizungumzia kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye mapema asubuhi.

No comments:

Post a Comment