TTCL

EQUITY

Friday, May 20, 2016

Wadaiwa Mikopo Elimu ya juu waongezewa siku 30,kuanzia leo Mei 20, baada ya hapo kubanwa kisheria


DSC_3873 
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo wakati wa tukio hilo la juu ya tathimini ya notisi ya siku 60 kumalizika na kuongeza siku zingine 30, zinazoanzia leo Mei 20. wengine ni viongozi wa bodi hiyo akiwemo Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo  Bw. Robert Kibona na Meneja wa Habari , Elimu na Mawasiliano  Bw. Omega Ngole (kulia). Wengine ni wanahabari wakifuatilia tukio hilo.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeamua kuongeza siku Thelathini (30) ilikutoa fursa kwa wanuifa na waajiri waliobaki kujitokeza  kulipia madeni yao waliokopa kupitia bodi hiyo, kuanzia 1994 hadi hivi sasa.
Wakizungumza na waandshi wa Habari mapema leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw. Robert Kibona alisema kuwa tathimini ya agizo la siku 60 kwa wadaiwa na waajiri limekwisha na wamejitokeza wa wingi licha  ya kuwapo na wengine walioomba kuongezewa muda kwa siku za kufanya hivyo ilikuweza kujitokeza.
“Machi 14 mwaka huu tulitoa notisi ya siku 60 kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu ta juu kujitokeza na kuanza kurejesha na Mei 13, 2016 siku hizo sitini (60) zilikamilika.

 
Wadau watatu muhimu ambao Bodi inawatambua kutokana na sharia ya Bodi ya  (SURA 178) ni pamoja na Mnufaika, Mwajiri na Mdhamini mbao kisheria wanatakiwa kurejesha mikopo hiyo baada ya miezi 12 tu ya mnufaika kumaliza elimu yake, hivyo mwitiko kwa wanufaika na waajiri ulikuwa ni mkubwa  kwa kujitokeza kujua madeni yao na kulipa” alisema Bw Kibona.
Wanufaika 2,007 ambao wanadaiwa jumla ya Tsh 1.93 Bilioni waliwasiliana na bodi ya Mikopo kwa njia mbalimbali ikiwemo kufika katika ofisi hizo. Pia waajiri 1528 waliweza kuwasilisha taarifa za wanufaika 19,714 ambao wanadaiwa Tsh 149.5 Bilioni. Hata hivyo jumla ya Wanufaika 21,721 ambao wanadaiwa jumla ya Tsh 151,5 Bilioni ambapo kati ya fedha hizo, kila mwezi wanatarajia kukusanya Tsh, 1.8 Bilioni  na hivyo kuongeza  kiasi cha ukusanyaji  kwa mwezi kufikia Tsh.8.0 Bilioni ifikapo mwezi Juni 2016.
Hata hivyo Bw. Kibona ameongeza kuwa, baada ya mwitiko kuwa mkubwa hivyo wameamua kuongeza siku hizo 30, ambapo baada ya hapo watachukua hatua kali za kisheria kwa wahusika wote waliooanishwa katika SURA ya 178.

No comments:

Post a Comment