TTCL

EQUITY

Saturday, May 21, 2016

Mwanafunzi Mbaroni Kwa Kumtukana Rais Wa Zanzibar Dkt.shein Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Mwamunyage.

 [​IMG]
Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya saa 09:00 asubuhi.

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku hakuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.

“Mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya 'Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti' hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “ alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtumiwa huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo, ”Dr. Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook."

Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na taratiu za kisheria.

Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily (40), mkazi wa Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakiku mkazi Arusha.

No comments:

Post a Comment