TTCL

EQUITY

Thursday, December 3, 2015

Wafanyabiashara, polisi waongoza kwa ufisadi Afrika

WAFANYABIASHARA wakubwa wametajwa kuwa miongoni mwa watu fisadi zaidi sawa na maofisa wa polisi Barani Afrika.

Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa na shirika la kuchunguza ufisadi duniani la "Transparency International" ambalo limebainisha kuwa raia mmoja kati ya watano barani Afrika hutoa hongo.

Ni mara ya kwanza wafanyabiashara kutajwa kuwa mafisadi wakubwa Barani Afrika na Shirika hilo limeongeza kuwa matumizi mabaya ya mamlaka yanasababisha ongezeko la umaskini pamoja na kuwanyima raia mahitaji muhimu.

Kwa mujibu wa Shirika hilo, watu wengi ambao ni maskini hujikuta mara kadhaa wakilazimika kulipa hongo ikilinganishwa na matajiri.

Nchi ya Liberia imetajwa kama inayoongoza kwa visa vya ufisadi Afrika huku ikifuatiwa na Cameroon, Nigeria na Sierra Leone.

Kwa upande wa Afrika Mashariki, Uganda inaongoza kwa visa vya ufisadi ikifuatiwa na Kenya huku Kusini mwa Afrika Zimbabwe na Zambia zikiongoza katika nchi zenye visa vingi vya ufisadi.

Botswana, Mauritius na Cape Verde ndiyo mataifa pekee ya Afrika ambapo visa vya ufisadi ni vya chini zaidi ikiwa ni asilimia mbili pekee. 

No comments:

Post a Comment