TTCL

EQUITY

Monday, December 14, 2015

Vijana 30 wapatiwa mafunzo uwekezaji Gesi asilia

Zaidi ya vijana 30 kutoka katika vyuo mbalimbali mkoani Mtwara wamepatiwa elimu juu ya masuala ya uwekezaji katika rasilimali za Mafuta na Gesi asilia, katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la MRENGO.
Baadhi ya mitambo katika Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia kutoka Songosongo na Mtwara kilichopo Somangafungu wilayani Kilwa Mkoani Lindi
 
Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo, baadhi ya wanafunzi hao wamesema imewasaidia kuweza kufahamu mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na namna rasilimali hizo zitakavyoanza kuwanufaisha wananchi ambao wengi wao wanatarajia kuona mafanikio kwa siku za karibuni.
Kwa upande wake, mratibu wa mradi wa Mafuta na Gesi unaotekelezwa na shirika hilo kwa kufadhiliwa na shirika la Utunzaji wa Mazingira Duniani (WWF), Mustafa Kwiyunga, amesema lengo la kuwajengea uwezo vijana hao ni kutaka kuendeleza majadiliano hasa katika vyuo mbalimbali na pia waende kuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu juu ya rasilimali hizo kwa wananchi.
Naye, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris (STEMMUCO) mkoani Mtwara, Justin Lusasi, amewataka wazizi na walezi kuhamasika katika kuwapeleka shule watoto wao kwa ajili kuwatengenezea misingi bora ya maisha ambayo wataipata kupitia rasilimali hizo, na waache kupoteza muda katika masuala ya Jando na Unyago.

No comments:

Post a Comment