TTCL

EQUITY

Monday, December 14, 2015

Mawaziri mtegoni

 

MAWAZIRI wapya walioteuliwa na Rais John Magufuli wameshauriwa kutekeleza majukumu yao mapya kwa kuguswa na matatizo ya Watanzania kama anavyoguswa Rais na sio wafanye kazi zao kwa nidhamu ya woga.
Wakizungumza kwenye mdahalo wa kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa bungeni hivi karibuni, ambao umeandaliwa na Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Tahliso), baadhi ya wasomi na wanazuoni walisema mawaziri wanapaswa kufanya kazi zao kwa dhamira ya kweli kutoka moyoni na sio kujionesha kwa Rais.
“Nawashauri wasifanye kazi kwa nidhamu ya woga, ila kama watafanya kwa kuguswa na matatizo ya nchi kama ilivyo kwa Rais watafika mbali; lakini kama wanafanya kwa nidhamu ya woga itakuwa ni nguvu ya soda,” alisema mtaalamu wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi.
Profesa Ngowi alisema mawaziri wakishindwa kutekeleza majukumu yao sio kwamba watakuwa wamemwangusha Dk Magufuli, bali watakuwa wamewaangusha Watanzania ambao ndio wanahitaji matunda kutoka kwa watendaji hao wakuu wa Serikali.
Alishauri pamoja na Dk Magufuli kuonesha dhamira ya kujenga reli, barabara na bandari, lakini ni vyema akajikita pia katika ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano kwa kuwa dunia yote inaelekea huko.
Dk John Jingu alizungumzia hoja ya kujenga viwanda nchini kuwa inawezekana kwani kuna nchi tajiri kama China zinatafuta kuhamisha ujenzi wa viwanda kwenda nchi zingine na akashauri Tanzania kutumia fursa hiyo kupitia sera ya mambo ya nje.
Pia alisema ujenzi wa viwanda utakuwa na faida kubwa iwapo ujenzi wa miundombinu kama reli utawasaidia wakulima kufikisha bidhaa zao kwenye masoko ya nje.
Alitoa mfano kuwa ujenzi wa reli kutoka Dar es Salama hadi Rwanda na nchi zingine za Maziwa Makuu utasaidia upatikanaji wa masoko wa bidhaa za alizeti inayolimwa katika mikoa inakopitia Reli ya Kati. Kwa upande wa kodi, alisema Dk Magufuli ameanza vizuri katika eneo hilo, kwani nchi inatakiwa kukusanya mapato yake ili wananchi wake ndio wapange vipaumbele ya taifa.
Alisema nchi ikitegemea wahisani katika mapato yake itatekeleza pia sera na vipaumbele vya wahisani hao. Kwa upande wake, Balozi Christopher Liundi alisema Dk Magufuli ni kiongozi na zawadi kutoka kwa Mungu kwani anachosema ndicho anachosimamia.
Alisema mawaziri wake ambao amewateua wanatakiwa waige kasi hiyo katika utendaji wake, lakini pia wafanye kwa dhamira ya dhati ya kuisaidia nchi.

 
“Mawaziri wakienda na kasi yake, Rais atapumua na atapata muda wa kushughulikia matatizo mengine ya nchi,” alisema Balozi Liundi na kuwataka Watanzania wamuunge mkono kwani kiongozi huyo sio malaika, bali ni binadamu mbaye wakati mwingine anafanya makosa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliyehudhuria mdahalo huo, Paul Makonda alishauri mfumo wa elimu nchini ufumuliwe kwa maelezo kuwa unazalisha watendaji wabovu ambao wanatoa huduma hafifu na za ovyo kwa wananchi.
Alisema watendaji wengi hawana ubunifu ambao unalenga kuokoa fedha za umma. Alishauri pia viwanda vitakavyojengwa visaidie kupunguza tatizo la ajira na akaonya kuwa kama Serikali haitakuwa makini wawekezaji wanaweza kuleta viwanda; lakini kazi ikawa inafanywa na maroboti na hivyo kutofikia lengo la utoaji wa ajira ambalo serikali inalenga.
Makonda aliyesema amehudhuria kama mwananchi na sio kama DC, alisema Tanzania ni tajiri ila fedha nyingi zinazotengwa na Serikali kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali inaishia kwenye mifuko ya wananchi wachache na akasema amelishuhudia Wilaya ya Kinondoni ambako barabara nyingi zilizojengwa kwa lami ziko chini ya kiwango.
“Kwenye mapambano haya ya kupambana na rushwa, hata akifinywa baba na mama yako kaa kimya ili tuweze kufika,” alisema Makonda.
Chisaye Robert alisema busara za Dk Magufuli zibadilishwe ziwe sheria ili hata akiondoka madarakani falsafa yake iendelee. Pia alimshauri afumue mikataba ya madini na kuwepo na uwazi kwenye mikataba hiyo kuona namna nchi inayonufaika.
“Namshauri pia awekeze zaidi kwenye elimu, sio kusomesha watu wengi, bali kwenye ubora wa elimu inayotolewa kwenye vyuo vyetu vikuu ili waweze kukidhi mahitaji ya soko ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema.
Awali mdahalo huo uliofunguliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye nusura uvunjike baada ya uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupinga kufanyika chuoni hapo kwa maelezo kuwa Tahliso inashindwa kusimamia masuala ya wanafunzi hasa mikopo.
Walitaka kwanza Tahliso ishughulikie mikopo ya wanafunzi ambao walisema wengi hawajapata katika vyuo mbalimbali na sio kuandaa mdahalo wa kujadili hotuba ya Rais Magufuli ambayo itajadiliwa na wabunge. Vurugu hizo zilizimwa na Nape ambaye aliwataka Daruso kama wana malalamiko ya Tahliso kumaliza matatizo yao kupitia vikao.
“Kama mnaona viongozi wa Tahliso hawashughulikii matatizo yenu waondoeni ila nawaomba tuache mdahalo huu ufanyike,” alisema Nape.
Alisema kama kuna wanafunzi ambao hawajapata mikopo, leo CCM itafuatilia suala hilo kwa kutuma mtu kwenye Bodi ya Mikopo.
“Bahati nzuri mimi bado ni Katibu Mwenezi wa CCM iliyoiweka serikali madarakani, kwa hiyo hilo tutaenda kulifuatulia kujua kwa nini baadhi ya wa

No comments:

Post a Comment