TTCL

EQUITY

Monday, December 14, 2015

Lema achukua tena Jimbo la Arusha Mjini


Uchaguzi mkuu wa ubunge katika jimbo la Arusha mjini umefanyika kwa amani, huku idadi ya wapiga kura waliojitekeza ikiwa ndogo kulinganishwa na chaguzi zilizopita.

Uchaguzi huo ulifanyika ikiwa ni zoezi la kukamilisha uchaguzi mkuu octoba 25 mwaka huu, kufuatia kifo cha mgombea wa ubunge wa chama cha ACT wazalendo Estomih Mallah, aliyefariki siku chache kabla ya uchaguzi.

 Msimamizi wa Uchaguzi kata ya Themi, Esther Kashangaki 
Wapigakura waliondikishwa kwenye daftari katika jimbo la Arusha Mjini ni laki tatu kumi na saba elfu mia nane na kumi na nne huku taswira ya awali ikionesha idadi ndogo ya wapiga kura tokea kufunguliwa kwa vituo saa moja asubuhi hadi kufungwa kwake majira ya saa kumi jioni.
Wagombea walioshiriki katika uchaguzi huo ni pamoja na Godbless Lema wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema aliyetetea kiti hicho na kufanikiwa kushinda kukitetea kiti chake cha ubunge tena baada ya kuongoza kwa miaka mitano.
Mgombea mwingine ni Philemon Mollel kupitia CCM aliyepiga kura katika kituo cha shule ya sekondari kimandolu kata ya kimandolu.
Zuberi Mwinyi mgombea kupitia chama cha wananchi Cuf aliyepiga kura katika kituo cha YMCA daraja mbili.
Mwingine ni mgombea pekee mwanamke Navoi Mollel kupitia chama cha ACT Wazalendo aliyepiga kura katika kituo cha Burka shuleni katika kata ya Olasiti.
Katika uchaguzi huo uliofanyika katika vituo 721 kwenye kata 25 za jimbo la Arusha mjini, baadhi ya wapiga kura wamesema mazingira ya zoezi hilo yalikua tulivu.
Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Mh. Godblees Lema ameibuka Mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya Siasa Mh Lema amepata kura 68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mgombea wa CCM Bw Philemon Mollel aliyepata kura 35.907 sawa na asilimia 34.4.
Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Mh Godblees Lema ameibuka Mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya Siasa Mh Lema amepata kura 68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mgombea wa CCM Bw Philemon Mollel aliyepata kura 35.907 sawa na asilimia 34.4.
Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Pamoja na Navo Mollel wa ACT Maendeleo aliyepata Kura 342 sawa na asilimia 03, Zuberi Mwinyi wa CUF aliyepata kura 106. Sawa na asilimia 0.1, na Makama Rashidi wa NRA aliyepata kura 43 sawa na asilimia 0.04.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Bw Juma Iddy, jimbo la Arusha wapiga kura walioandikishwa ni 317.814, na waliojtokeza kupiga kura ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 na kura halali ni 104,353.

No comments:

Post a Comment