TTCL

EQUITY

Monday, April 14, 2014

Ndege, Wanyama na Wadudu Wametuzidi Kiakili...Ona Ufuska Huu!!!!



Mimi ni mpenzi sana wa semina za Dk. Ndodi ambaye hutoa elimu juu ya mambo mbalimbali ikiwemo elimu juu ya lishe bora ambayo hutoa mara kwa mara katika vyombo vya habari.  Siku moja nilimsikia akisema kuwa panya wanamzidi binadamu akili kwa sababu katika mbegu za mahindi huwa anakula viini vya ndani vya njano ambavyo ni sehemu mzuri katika mahindi. Cha kustaajabisha, binadamu anayejiita mwenye akili kuliko viumbe wote anavitoa viini hivyo kabla ya kuyasaga hayo mahindi ili kupata unga wa ugali!!!!!

Msemo wa Dk. Ndodi  ninauunga mkono kwa asilimia 100 kwani nimegundua si  Watanzania peke yake wanazidiwa akili na wanyama, ndege na wadudu bali hata wazungu nao wamelidhihirisha hili kwa sasa. Haiwezekani na haijawahi kutokea kuwa wanyama, wadudu, na ndege wenye jinsia moja wametakana kimapenzi. Ikitokea umemuona jogoo akimpanda jogoo mwenzake ama temba anampanda temba mwenzake, jua dunia imefika mwisho.

Binafsi ninasikitishwa sana na kitendo cha wazungu kuhimiza kukubalika kwa ndoa za jinsia moja – eti wanaume waruhusiwe kuoana na wanaume wenzao na wanawake pia waoane na wanawake wenzao! Hili linadhihirisha kuwa binaadamu hawana akili…

Kwa sasa nimeanza kutilia mashaka ule msemo wa kuwa binadamu ndiye kiumbe mwenye akili kuliko viumbe wote. Hatuwezi kusema hivyo tena kutokana na mambo ya kipuuzi tunayoyafanya na kuyashadadia, na ambayo hayajawahi kufanywa na mnyama, ndege ama mdudu yeyote ingawa tunadai kuwa  hawana akili.

Vitabu vya dini vinatuambia kuwa Mungu alituleta duniani ili tuoane na kuongeza dunia kwa kuzaa binadamu wengine. Sasa swali langu litabakia palepale kuwa watoto watatoka wapi ikiwa wanaume kwa wanaume na wanawake kwa wanawake wanaoana, na hili limehalalishwa duniani kote na Mabepari wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini?

Na ukumbuke katika vitabu hivyo hivyo vya dini, Mungu aliwaadhibu vikali Wasodoma na Wagomora walioyafanya haya haya ambayo kwa sasa yamehalalishwa. Hili linadhihirisha ni makosa makubwa sana.

Nina kuhakikishia itafika kipindi sheria itaanza kutetea wazee wanaowabaka watoto wao kwa msemo huo huo “ Uhuru na Haki za Binadamu

Mdau, unalizungumziaje hili suala wewe???

No comments:

Post a Comment