TTCL

EQUITY

Thursday, March 13, 2014

HUU NDIO UKATILI WANAOFANYIWA MASHOGA WA UGANDA


ikiwa ni Ni siku chache tu toka Uganda ipitishe sheria ya kupinga ushoga, imeripotiwa mtu mmoja aliyetuhumiwa kuwa shoga alichomwa moto mpaka kufa nchini humo.
CNN imeripoti tukio hilo ambalo jina la mtu  huyo halikuweza kujulikana. Picha ilionesha jinsi mtu huyo anavyochomwa moto huku akiwa pembeni mwa reli huku watoto wakishuhudia tukio hilo.
Sharia hiyo iliyopitishwa hivi karibuni, inahusisha pamoja na kufungwa maisha kwa mtu yoyote atakayejihusisha na shughuli zozote za ushoga pamoja na kuambukiza ukimwi, matendo ya ngono na watoto pamoja na watu wenye ulemavu, udhalilishaji ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Sharia hiyo iliyozaliwa mwaka 2009, na kupewa jina “Kill The Gays” ikimaanisha “Ua Mashoga” ambayo ilisisitiza hukumu ya kifo kwa matendo fulani ya ushoga, lakini ilirudishwa kabatini kutokana na kelele nyingi zilizopigwa na mataifa mbalimbali.
Katika sharia hii mpya, mtu yeyote atakaye fungisha ndoa ya jinsia moja atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka 7. Atakayeshindwa kutoa taarifa ya ushoga polisi pia ni mualifu.
Madaktari watakao watibu mashoga, watakaopangisha mashoga kwenye nyumba zao na wale wataka shukiwa kuwa mashoga, wasagaji, waliobadilisha jinsia na mabasha watafungwa miaka 5.
Mtu yeyote atakayetoa msaidia kwa shoga atakuwa anavunja sharia, ambapo atachukuliwa hatua.
Watu wengi wanaamini kuwa sharia hii ni muhimu ili kupinga tabia na tamaduni za nchi za magharibi. “ hii sharia ni muhimu kwa nchi hii ili kulinda tamaduni za Mwafrika” alisema David Bahati ambaye ni mbunge ambaye aliuwakilisha muswada huo bungeni.
Bahati pia ni mmoja kati ya kundi linalotuma fedha katika nchi za Afrika kuunga mkono wanaopinga shughuli zote za ushoga.

No comments:

Post a Comment