Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema, machungu ya mgawo wa umeme
unaoendelea sasa yatapungua kuanzia leo baada ya kukamilika kwa
asilimia 85 ya matengenezo ya Kisima cha Gesi cha Songosongo mkoani
Lindi.
Matengenezo
ya kisima hicho yaliyoanza Novemba 16 mwaka huu, yamesababisha kushuka
kwa uzalishaji wa umeme na hivyo kuathiri shughuli mbalimbali za
uzalishaji na huduma za jamii.
Meneja
Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alisema, hatua hiyo inatokana na
kuzimwa kwa mitambo ya Kampuni ya Pan African iliyoko Songosongo ili
kuruhusu matengenezo.
Alisema
mgawo huo ulipaswa kuwa wa saa mbili lakini imeshindikana kwa sababu
nishati hiyo inakosekana kwa zaidi ya saa 12 kila siku.
Badra alisema maeneo yanayoendelea kuathirika ni Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Tanga, Arusha na Zanzibar.
Hali kadhalika mikoa mingine kadhaa.
Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema kupungua kwa mgawo huo kunatokana na matengenezo ya visima vya gesi.
Alisema
shirika linatarajia kupokea asilimia 80 ya gesi kuanzia jana jioni,
tayari kwa uzalishaji wa umeme na kwamba hatua hiyo itaongeza
upatikanaji wa nishati katika maeneo yaliyoathirika.
“Mgawo utapungua kutokana na kiasi cha asiliami 80 ya gesi kitakachoanza kuingia leo (jana),” alisema.
Visima
vya Songosongo siyo mali ya Tanesco, Tanesco inanunua gesi kutoka kwa
Songosongo ambao wakiwa na matengenezo wanatupa taarifa tu,” alisema
Mramba.
No comments:
Post a Comment