TTCL

EQUITY

Tuesday, November 26, 2013

HII INAKUHUSU HATA KAMA HUTAKI!!

MAPROFESA WABAINI TEKNOLOJIA MPYA YA KUBAINI CHANZO CHA KIFO CHA BINADAMU, SASA SUALA LA KUMPASUA MAREHEMU ILI KUBAINI CHANZO CHA KIFO LITAKUWA HISTORIA.

File:US Navy 030819-N-9593R-125 Hospital Corpsman 2nd Class Roy Puerto, right, of Olangapo City, Philippines, demonstrates the operation of the CT Scan machine.jpg
 
WAKATI mageuzi yakiendelea kwenye   ulimwengu wa sayansi na teknolojia,  wataalamu hawajalifumbia macho tatizo  la utata wa baadhi ya vifo.

Waliobobea katika eneo hilo la kuchunguza maiti ili kubaini
kilichomsababishia mhusika mauti, sasa wamekuja na mbinu mpya, ambapo si lazima tena kumpasua marehemu kama ilivyozoeleka. Kwa misingi hiyo, wale watu wenye ‘nyoyo ndogo’ waliokuwa
wanajihisi vibaya marehemu wao kupasuliwa, wengine kwa imani
kwamba kuna kitu kinatolewa huko, sasa watapata pumziko walau kwa upande huo.


Njia mpya sasa ni kuuangaza mwili kwa mwanga wa kompyuta, wenyewe wakiita CT Scanner, ili kuchunguza kilichosababisha kifo. Njia hii inatumika pia kubaini viungo vya mwili vilivyovunjika, kuteguka au hata ikiwa mtu ana aina fulani ya ugonjwa ambao
mashine husika inaweza kuubaini. 


Pamoja na picha hiyo kupigwa maeneo yanayotakiwa katika mwili wa marehemu, tishu au ogani kwenye shingo huchomwa kidogo tu ili kufanikisha ufuatiliaji wa mishipa, na kukamilisha uchunguzi huo.

Teknolojia hiyo ya kisasa zaidi, wataalamu wanasema, imeshafanywa mara kadhaa na matokeo yake yamekuwa ya uhakika kwa asilimia 80 kwenye kung’amua chanzo cha kifo.

Hiyo ni hatua kubwa na muhimu kwenye eneo hilo kwa madaktari, kwa sababu itaondoa adha iliyokuwa imezoeleka siku na miaka iliyopita, ya kupasua mwili wa mhusika ili viungo nyeti, si vya siri, vipate kukaguliwa na hatimaye wataalamu wabaini kilichosababisha kifo. 


Uvumbuzi huo umefanywa na Chuo Kikuu cha Leicester, kilichopo jijini Leicester, Leicestershire nchini Uingereza. Kiongozi wa wataalamu hao ni Profesa Guy Rutty. Kwa ugunduzi huo, ni wazi kwamba, walau kwa wakati ujao katika hata nchi zote itakuwa rahisi kupata uamuzi unaokubalika kuhusu nani alifia wapi na kipi chanzo cha kifo chake na huenda utata unaokumba vifo vingi sasa ukafutika.

Utamaduni katika nchi nyingi, zikiwamo Marekani na Uingereza, umekuwa ni kwamba baada ya vifo polisi ndio wanachunguza sababu zake, na hata pakiwa na utata, korti husimamia, huku ofisa anayechunguza vifo na kutoa vyeti vyake (coroner) akisubiri tu kutoa taarifa yake kama kubandika stempu kwenye bahasha au kupiga muhuri kugusa stempu na bahasha yake.

Professor Bruno Giuranna.

Ugunduzi huo bila shaka utabadili taratibu, na si ajabu hata sheria na kanuni zikabadilishwa, ili kuokoa muda na kuondoa kutofautiana kati ya watu kwenye masuala hayo yamekuwa yakichukua muda mrefu na kuwaacha ndugu katika majonzi kwa kufuatilia mambo ya mpendwa wao, huku ikijulikana wazi kwamba hatarejea kwenye dunia hii, hata iweje.

Tayari Profesa Rutty ametunukiwa tuzo na mamlaka husika, kwa sababu ya kazi yake hiyo, aliyoianza muda mrefu uliopita, akiipa jina ya ‘Operesheni Tochi’. Wataalamu wanasema kwamba, teknolojia hiyo mpya itatumika kwa ufasaha katika kuchunguza sababu ya vifo vya kawaida na vile visivyo vya kawaida, iwe kwa mtu mmoja au hata kwa wengi wanaokufa kwa wakati
mmoja.

Tena, teknolojia hii itakuwa habari njema kwa watu walio kwenye makundi ya kiimani, ambayo kwa miaka kadhaa sasa, wamekuwa wakipinga upasuaji wa wafu ili kubaini sababu ya vifo vyao.
Profesa Rutty na wasaidizi wake katika mradi huo tayari wamechapisha mada ya kazi yao kwenye jarida la kimataifa la
masuala ya afya liitwalo ‘International Journal of Legal Medicine’.

Humo wameeleza teknolojia waliyotumia kufikia mafanikio hayo na protokali iliyofuatwa tangu kwa mtafiti mmoja huru hadi mwisho, chini ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Afya (NIHR) ya Uingereza. Profesa Rutty aliye kwenye kitengo cha utafiti wa saratani chuoni
Leicester, anasema kwamba utafiti huo utasaidia sana na kubadili jinsi ya kushughulikia maiti katika kipindi kijacho. 


Kwamba uchunguzi wa maiti si kitu cha kawaida sana au kinachofuatiliwa kwa karibu na watu wengi, na pia wapo ambao wamekuwa wakichukia watu wao, kwa maana ya ndugu, rafiki au
wana dini au itikadi moja kupasuliwa baada ya kufariki dunia.


“Kabla ya utafiti huu, pasipo kutumia angiografia, vifo vitokanavyo au kuhusishwa na matatizo ya moyo havikuweza kuchunguzwa na kupatiwa sababu kwa uhakika kwa njia ya utafiti (Post mortem) kwa CT Scan, kwa hiyo tulihitaji kutafiti na kubaini mfumo ambao ungetuwezesha kufanya hivyo,” anasema, huku akifurahia kufanikiwa kupata mfumo wenyewe. 


Profesa Rutty alishirikiana na Profesa Bruno Morgan na wengine kwenye kitengo cha radiolojia, na wakabuni na kufanikisha mfumo wa kumchoma marehemu kidogo tu shingoni wakati wa kuchukua picha hiyo kwa kompyuta (scanning).

“Kuchoma huko husaidia kufuatilia moja kwa moja mishipa ya moyo, ni teknolojia isiyo ghali, rahisi kuifanya na yaweza kutumiwa kwa aliyefariki dunia kwa kifo cha kawaida na kisicho cha kawaida,
cha mtu mmoja au cha watu wengi,” inasema taarifa ya Chuo Kikuu cha Leicester kwa vyombo vya habari.


“Tulikuwa kitengo cha kwanza duniani, kwa kutumia elimu yetu, kupendekeza matumizi ya angiografia kama njia ya kuepukana na aina zilizopitwa na wakati za kutafiti chanzo cha vifo, na pia ni wa
kwanza kuweka bayana maendeleo yake... makundi mengine yamefanya angiografia ya mwili mzima ambayo huchukua muda mrefu, ni ghali na si rahisi kutekelezwa kwenye uchunguzi wa kila siku katika Uingereza,” Profesa Rutty anajigamba.

Mada nzima ya utafiti iliyowasilishwa na kuchapwa, inaonesha matokeo ya majaribio 24, huku timu nyngine ya Chuo Kikuu ikipewa jukumu la kupitia mengine 200, ili kupitia teknolojia
tuliyotumia na kujenga msingi mkubwa zaidi wa ushahidi. Matokeo ya utafiti huu hayakupokewa kimya kimya, yalikuja na mwangwi kutoka kwa wataalamu na wasio wataalamu kadhalika.

Mmojawapo ni kutoka nchini Marekani. Huko, Mohit Joshi, akiwa Washington, makao ya serikali, akiliandikia jarida liitwalo ‘International Journal of Legal Medicine’, anasema wanasayansi wa
Uingereza wamegundua teknolojia kubwa, lakini itakayotumiwa kirahisi. 


Kwamba teknolojia hiyo ni mapinduzi makubwa kwenye utafiti wa vifo na itapunguza gharama za awali zilizoingiwa na watu na taasisi mbalimbali kubaini sababu za vifo. Joshi, pia, anagusia kwamba ugunduzi huo utatoa faraja kwa vikundi vya imani visivyopenda maiti kupasuliwa.
 
 http://news.bbcimg.co.uk/media/images/66215000/jpg/_66215004_pounder.jpgProfesa Derrick Pounder.
 
Ilitarajiwa kwamba, England na Wales zingepunguza haraka idadi ya utafiti wa vifo kwa kutumia njia ya zamani, kwa asilimia 60. Profesa Derrick Pounder anasema kwamba kiwango cha utafiti wa maiti 110,000 coroner kwa kila maiti 500,000 ni kikubwa, kwa hiyo kwa kutumia teknolojia hiyo mpya itakuwa rahisi.

Akiandika kwenye jarida la ‘Royal Society of Medicine’, anasema kwamba katika Scotland ni asilimia sita, ikilinganishwa na 22 ya England na Wales. Hata hivyo, Profesa Pounder anayetoka Chuo Kikuu cha Dundee, anashangaa sababu ya watu wengi kiasi hicho wanataka kuchunguza sababu za vifo.

Haoni kwa nini, hufika mahali serikali ikaingilia mambo ya kifamilia na kuagiza uchunguzi wa maiti wengi kubaini sababu za vifo vyao. “Japokuwa utafiti wa ndani ni zana muhimu kwenye uchunguzi wa kisasa wa sababu za vifo, si sahihi kila kifo kukifanyia uchunguzi
kiasi hicho. maiti wachunguzwe pia kwa kuangaliwa nje, ni gharama nafuu. 


Kuwe na uwiano kati ya uchunguzi unaoagizwa na serikali na ule wa ndugu au wadau,” anasema.
http://manyandahealthy.blogspot.com

No comments:

Post a Comment